face

Dola ya Kiislamu

Dola ya Kiislamu

Dola ya Kiislamu

Marafiki watatu walipoanza kikao chao Maiko na Rajev walisikia sauti zenye kuingilia sauti ya Rashidi, walipouliza Rashidi aliwajulisha kuwa sauti hiyo ilikuwa ni taarifa ya habari, na wakasubiri hadi dakika kadhaa ilipokwisha….baada ya muda mfupi Rashidi alianza kuzungumza.”

Samahani, nadhani mtanisamehe, najua mnajua umuhimu wa mtu kusikiliza taarifa ya habari siku hizi, kwa uchache kwangu…Je mnafuatilia kinachotokea kwenye nchi yangu siku hizi?

Rajev: Ndio, ni habari za kusisimua, matukio ya haraka haraka yenye kufuatana.

Maiko: Huenda kitu kikubwa kilichonivutia mimi ni kujitokeza kwa wanaoitwa Islamiyuun (Waislamu sana) na jaribio lao la kubadilisha mfumo wa nchi ili uwe wa Kiislamu….ni jambo lenye kutisha.

Rashidi: Kinachosumbua ni nini katika hilo.

Maiko: Dola za watu za kidini, zime jaribu nchi za kidini na imethibitika kufeli kwake, yalikuwa ni majaribio machungu; dola za kidini zimekoma zama zake tokea karne za kati.

Rashidi: Lakini unakusudia nini kusema dola ya kidini?

Maiko: Ni dola ambayo tabaka lenye kuhukumu linakuwa chini ya watu wa dini ambao wanadai kuwa wanazungumza kwa jina la Mungu. Miongoni mwa mambo muhimu katika dola ya kidini ni kuwa zinatoa haki kwa jina la Mungu na hili linarejea kwa kuwa wao wanazungumza kwa jina la Mungu; hivyo hujiweka katika nafsi zao katika muktadha wa sifa ya kuepushwa na madhambi na utukufu; na hupelekea hilo kudai kuwa wanaopinga utawala wao wanapingana na Mungu, na wao hawahesabiwi wala kuulizwa na yeyote.

Rashidi: Kwa bahati mbaya kuna tatizo la taswira tofauti dhidi ya dola ya Kiislamu, mimi naafikiana nawe kukataa sura hii uliyoitaja, na huitwa ‘Theocratic’, Lakini theocratic ni mfumo wa kutawala ambao unachukua nguvu yake (na sio tu kwenye mfumo wa sheria zake) kutoka katika dini;……ikiwa Ulaya imepata shida ya utawala huu chini ya mikono ya kanisa katika zama za kati, basi Uislamu haukujua sura hii na haujakubaliana na hali kama hii, katika Uislamu hakuna utawala wa watu wa dini, lakini kuna utawala wa dini chini ya watu wenye kufanya makosa na wenye kupatia, na wenye kuhesabiwa na kuadhibiwa, na wanauzuliwa ikibidi kufanya hivyo, kiini cha tofauti hapa ni kuwa dola ya Kiislamu rejea yake ni Uislamu na utekelezaji wake ni watu wenyewe, watu ambao hawamiliki utakatifu, hakuna katika Uislamu mtawala ambae anadai kuwa anapokea sheria zake na utawala wake kutoka kwa Mungu (baada ya kuzungumza nae) bali hapana budi umma wenyewe ushiriki.

Kama ambavyo uzoefu wa ulimwengu wa Kiislamu kuhusu dola ya Kiislamu ni uzoefu uliofanikiwa, uliopata maendeleo kwa wakati wake, kinyume kabisa na uzoefu wa dola za kidini Ulaya.

Rajev: Tumejua tofauti kati ya dola ya Kiislamu na dola ya kidini; sasa ni ipi tofauti iliyopo baina ya dola ya Kiislamu na dola isiyokuwa ya kidini?

Rashidi: Tofauti ni kubwa na za kimsingi kabisa, ninachokijali zaidi ni msingi wa tofauti yenyewe, ambayo inajificha katika tofauti kati ya taswira ya Uislamu na taswira ya kisekula ya ulimwengu, maisha na mwanadamu, mfumo wa dola katika Uislamu unatoka katika taswira ya Uislamu ambayo dini na maisha yanashikana, na hupamba mfumo uliokamilika anaoishi Muislamu, na kukamilika ndani yake nafasi ya mtu, umma na dola.

Ili tudiriki hayo ni juu yetu kudiriki kuwa: Ni ipi nafasi yetu ya kweli katika mamlaka ya Allah? Ikiwa tutakiri kuwa Mwenyezi Mungu ndie aliyetuumba basi kwa kawaida sisi hatuna hadhi yoyote isipokuwa kufuata radhi zake tu, na ikiwa tutakiri kuwa ardhi hii na mbingu hizi ni miliki yake pekee, inapasa tukiri kuwa haifai atakayepita katika miliki yake isipokuwa kwa utashi wake tu, na ikiwa tutakiri kuwa Mwenyezi Mungu pekee ndie anayetulea, na yeye pekee ndie ambaye anaturuzuku, hatuna nafasi sisi isipokuwa ni kuwa watumwa wake…..na ikiwa Allah ndie mwenye kutuhukumu na mwenye kuhukumu kila aliye katika ulimwengu huu, hatuna nafasi ya kweli hapa ulimwenguni isipokuwa ni kuwa katika ukamilifu wa utukufu wake na unyenyekevu kwake.

Maiko: Lakini, nini kinachotuita katika kurejea uzoefu ule kama sio hadhari na maneno, mwanadamu anaweza kuamua mwenyewe vipi ataishi, na kipi ambacho kitampelekea kwenye furaha yake, na ni umbo lipi litafaa kupanga maisha yake, kisha baada ya hapo hakuna ubaya kufahamu ndani ya nafsi yake na kuendeleza uzoefu wake.

Rashidi: Ukweli wa mas-ala haya ni: Je, inafaa kwa mwanadamu kuwa mtu sahihi kwa utawala au uwekaji sheria au chanzo cha hukumu? Sisi tunajua kuwa chombo chochote ikiwa mtu mjinga atatawala kukiendesha basi bila shaka atakiharibu….Mathalani ikiwa mtu asiyejua kuendesha gari na yeye hafahamu hilo, tunajua hatima ya mpumbavu huyu, hebu tufikirie: Ikiwa hii ndio hali ya hiki chombo kidogo cha chuma inashindikana kukiendesha bila ya maarifa sahihi, iweje iwezekane kwa mwanadamu ambaye hajijui sembuse kuwajua wengine atawezaje kusimamia uendeshaji wa chombo cha mwanadamu, kilichochangamana ndani?!

Maswala mengine: Ni kuwa hakuna njia ya kufikia uadilifu isipokuwa kwa kutotawaliwa uwekaji wa mfumo wa maisha ya mwanadamu isipokuwa watu ambao utu wao unalingana katika mtazamo wake, wala asiamue haki kwa wote isipokuwa yule asiyekuwa na tamaa za mali za watu, familia, tabaka au umma kwa sifa maalumu, uadilifu hauwezi kusimama ardhini isipokuwa kwa njia hii tu.

Na mwanadamu hawezi kuwa mtupu kwa mahitaji yake mwenyewe; huu ni udhaifu wa mwanadamu unaolazimiana na kila mwanadamu, tuwaangalie viongozi wa kisiasa na viongozi wa kidini katika Brahma na wa Kipapa na Masheikh wa twarika na watu wenye nafasi zao za fedha, tunawaona wote hao wakijipangia na kujiwekea nafasi nzuri zaidi na kujipendelea, hivyo basi kila kanuni iliyowekwa kwenye dunia hii na sheria chini ya utawala wao huwapa wao haki zaidi na kuwapendelea ambayo hawakupewa watu wengine, na huyafanyia mapambo na kuyafanyia sheria kwa njia nyingi, na kwa bendera zao huwadanganya watu kuwa hayo ni katika hali ya kawaida, Je inawezekana ikawekwa misingi ya dola adilifu na jamii iliyokuwa sawa katika jamii ambayo hutawaliwa na watu kama hawa?!

Tuangalie dola kubwa ambazo zimetumikisha umma zingine ambazo zinategemea nguvu zake; ni kanuni ipi miongoni mwa kanuni, au mfumo gani miongoni mwa mifumo ambayo athari yake haisambai kwenye mishipa yake. Je, hutarajiwa kwa watu hawa wawawekee wanadamu mfumo au sheria ambazo zitasimamia misingi ya haki na uadilifu?!

Rajev: Lakini bwana Rashidi mnafanya nini katika dola ambayo kuna wana dini wengine ambao ni wachache ambao sio Waislamu….kwa mfano sisi India, kuna dini zenye watu wengi lakini ni wachache (kulinganisha na Wahindi). Nyie mnapofanya rejea ya dola kuwa ni Uislamu mnalazimika kukubali dini ambayo si yenu.

Rashidi: Vizuri umenikumbusha jambo hili, pana nukta tatu ningependa kuweka bayana katika suala hili:

Ya Kwanza: Nawashangaa mnakataa mtu asiyekuwa Muislamu kuishi chini ya kivuli cha dola ambayo rejea yake ni Uislamu pamoja na kuwa dini yake haiti kwenye kusimamisha dola yake maalumu katika ardhi…wakati ambapo mnawalazimisha Waislamu kutii mifumo inayokwenda kinyume na dini yake na kukubali rejea ambazo zina kwenda kinyume na itikadi yake pindi anapoishi katika dola ya kisekula, pamoja na kuwa dini yake haikubaliani nayo.

Ya Pili: Uislamu kufanywa kuwa ni rejea ya dola haina maana kulazimisha Uislamu kwa wasio waislamu, na kikwazo hiki kimeibuka kutokana na taswira ya usekula kwa dini ambayo inaiona kuwa mipaka yake inaishia kwenye itikadi yake yeye mwenyewe ndani ya nafsi yake, wakati ambapo Uislamu hauishii hapo; Uislamu kulingana na Muislamu ni itikadi na sheria (yaani ni mfumo na kanuni) na ni rejea ya Ustaarabu, ama asiyekuwa Muislamu anaweza kuuchukua Uislamu kama ni ustaarabu na kuwa chini ya mfumo na kanuni zake, bila kuingia katika itikadi na ibada zake, haswa haswa kama mnavyozungumza kuhusu uwezekano wa kutekeleza Uliberali na Ujamaa katika jamii ambazo hazikuibukia katika mambo hayo na kwa wafuasi wa dini na mila nyingine.

Ya Tatu: Kusimama kwa dola ambayo rejea zake ni za Kiislamu haina maana kumeza haki za wachache au kuingilia katika hukumu maalumu za kidini kwao, Uislamu unadhamini haki za wachache, wala haikatazi wao kuhukumiana katika dini zao na katika mambo yao maalumu.

Maiko: Lakini sisi hivi sasa tunaishi katika zama zisizokuwa zile ambazo Uislamu uliibukia, ukatekeleza na kusimamisha dola yake, hata kama juhudi hizi zitafanikiwa tutahesabu kuwa ni hatua ya kurudi nyuma…ni hatua ya kukosa maendeleo; kwa hili nyie mnataka sisi tuhame fikra zetu na tusimamie mambo ambayo leo hii hayakubaliki wala hayana mantiki yoyote pamoja na maisha mapya.

Nyie kwa mfano bado mnashikilia kuharamisha riba, na hilo ni jambo muhimu katika uchumi hakuna nchi leo hii inaweza kuiacha.

Rashidi: Ewe rafiki yangu maneno yako kwa mfano huu na mifano mingine imejengeka katika misingi isiyokuwa ya kweli, leo hii taswira ya mfumo wa dola na utaratibu wa ulimwengu ambao tunaishi baada ya kulazimisha mfumo huu (riba) na kupuuzia athari zake hadi kwa kuwafanya wanadamu wafungamanishe mfumo wa uchumi na riba.

Ni kweli Uislamu umeharamisha riba, lakini sio sahihi kuwa riba ndio msingi wa uchumi.

Mabepari ndio waliolingania riba na ndio walimbikizaji ulimwenguni, na wanawadanganya walimwengu kuwa uchumi bila riba hauendi, ukweli ni kuwa hauendi katika ulimwengu wa mabepari, pamoja na hayo wana uchumi wakubwa katika ulimwengu wa Magharibi (mabepari) sasa hivi wanapinga mfumo wa riba na wanasema kuwa matokeo yaliyohitimishwa kwa vizazi vingi ni kuangukia katika matatizo ya kiuchumi na ya kifedha, na matatizo ya kijamii yanayoifuatia kwa sababu ya kuuweka uchumi mikononi mwa watu wachache tu, na kuwanyima watu wengi katika jamii, na ni haki yetu kuangalia matatizo ya madeni ya majengo na matatizo yaliyofuatia na balaa ulimwenguni, na kabla yake matatizo mengi, yaliyokuwa maarufu zaidi ni tatizo la: kuanguka kwa uchumi wa ulimwengu (Great Depression) katika miaka ya thelathini katika karne iliyopita ili tuweze kujua ukubwa wa tatizo hili.

Miongoni mwa miujiza ya mfumo wa Kiislamu ni kuharamisha riba na ulimbikizaji (nguzo mbili za mfumo wa ubepari) kabla ya kuibuka kwa rasilimali (mfumo) kwa miaka elifu moja. Rafiki yangu kwa hakika dola ya Kiislamu sio tu ni jambo la ulazima katika sheria ya Kiislamu, bali ni lazima vile vile kwa mwanadamu.

  - viambatano za migadala ya saada
  - viambatano za simulia
  - viambatano za vitabu
  - viambatano za vidio