face

Mustakbali wa Dini Hii

Mustakbali wa Dini Hii

Mustakbali wa Dini Hii

Rajev alichelewa (katika hali isiyokuwa kawaida yake) katika kikao na rafiki zake, na alitokezea katika Skrini ya Laptop, Maiko akaanza kuzungumza nae.

Halo! Rajev, umezoea kufika kwa wakati katika miadi yetu tunataraji kuchelewa kwako kusiwe ni kwa tatizo lililokusibu.

Rajev: Samahani rafiki zangu, hakuna neno, lakini nilishughulishwa kumalizia utafiti wangu ambao nilitaka kuwaonesha.

Maiko: Vizuri sana, kama ni hivyo mjadala utakuwa na faida kubwa, utafiti wako unahusu nini?

Rajev: Kwa hakika mjadala wetu wa mara kwa mara umenivutia sana na umenipa maarifa mengi kuhusu Uislamu, hivyo basi nikataka kufanya utafiti kuhusu kuchambua katika harakati ya kuenea kwa dini hii na kupanuka kwake ulimwenguni.

Maiko: Jambo hilo hilo limenivuta kufanya utafiti vile vile, lakini katika nyanja nyingine zinazohusika na kupanua utafiti wa nyanja ambazo tutaziangalia kwa undani zaidi na kutokana na vyanzo vyake vya asili….hata hivyo nini ulichokipata katika utafiti wako? bwana Rashidi!! je upo nasi??!

Rashidi: Ndio, ndio, nipo nafuatilia pamoja nanyi.

Rajev: Nimekuta marejeo na elimu nyingi zinaashiria kuzidi kupanuka kwa Uislamu ulimwenguni, utafiti umegundua kuwa kuwepo kwa zaidi ya mila na desturi 4,200 ulimwenguni, na takwimu zinathibitisha kuwa dini ya Kiislamu ndio yenye kuenea zaidi kati ya itikadi zote ulimwenguni! Na kuwa leo hii inasambaa mabara yote uliwenguni kwa haraka, tutakapoangalia kiwango cha ukuaji wa Waislamu na kulinganisha na ukuaji wa wafuasi wa Ukristo mathalani, unapata takwimu ya Umoja wa Mataifa inayosema:Kiwango cha ukuaji cha Waislamu ulimwenguni ni asilimia 6.4% wakati ambao cha Wakisto haizidi asilimia moja 1%.

Utafiti wangu umeangalia Ulaya, nikakuta Uislamu kwa mfano: Ndio dini ya pili nchini Hispania, Ufaransa na Uingereza.

Huko Ujerumani Waislamu wanaongezeka, na kulingana na gazeti la Die Zeit la Ujerumani la kila siku ni kuwa: Uislamu husambaa Ujerumani na kuongezeka kila siku.

Utafiti uliofanywa na wizara ya ndani ya Ufaransa umethibitisha kuwa: Zaidi ya watu 3,600 wanasilimu kila mwaka kama ambavyo inaashiria kuwa kuna misikiti 2,300 na Waislamu milioni 7, na kuna matarajio kuwa ifikapo mwaka 2025. Waislamu watafikia robo ya wakazi wote wa Ufaransa, wakati ambapo utafiti huo huo unaashiria kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na Waislamu asilimia 20% Ulaya, kadhalika kuna takwimu nyingine zinaona kuwa ifikapo mwaka 2040 Waislamu ndio watakaokuwa wengi Ulaya.

Takwimu zinasema kuwa theluthi ya wananchi wote wa Holland watakuwa ni Waislamu baada ya miaka kumi, na moja katika tafiti hizo zinathibitisha kuwa idadi ya Waislamu inaongezeka kwa kustaajabisha kwa raia wa Sweden, ambapo takwimu rasmi zinaashiria kuwa idadi ya Waislamu inaongezeka kila siku kiasi cha kufikia leo hii Waislamu 120 elfu.

Baada ya upanuzi wa misikiti ambacho ni kiashiria cha kusambaa kwa Waislamu, haswa wale walioshikamana na dini yao, tafiti hizo zinaonesha kuwepo kwa zaidi ya misikiti elfu 25 Ulaya pamoja na ongezeko la wenye kuswali katika misikiti hiyo miongoni mwa Waislamu.

Kwa mkabala tafiti zinathibitisha kupungua sana kwa wanaokwenda makanisani, utafiti uliofanywa na Dresdner Bank kuwa idadi ya wanaokwenda Makanisani huko Ujerumani imepungua katika miaka ya karibuni ambapo imetarajiwa kusimamisha misa za kidini katika makanisa 96 katika jumla ya makanisa 350 katika Essen Parish peke yake, na hivyo majengo ya kanisa kutumika katika malengo mengine, na hiyo ni kwa sababu ya kupungua wenye kwenda makanisani na kupungua kwa mapato ya kanisa.

Pengine kinachoonekana ni udhaifu mkubwa wa Wakristo kwenda makanisani mwao, kiasi cha hali hiyo kufikia katika kanisa moja katika nchi ya Ulaya lilifanya mashindano ya magari ili kuwavuta watu kwenye sala; kwa sababu ya uchache wa wenye kwenda kwenye makanisa.

Maiko: Hilo linaweza kufasiri tunachokiona katika zile hali ngumu za vyama vya mlengo wa kulia na baadhi ya wenye kasumba Ulaya kwa kuwabana Waislamu na kukebehi Uislamu Tuli zake na kuwafanyia uadui watu wake au nembo zao, bali kuwataka Waislamu wote waondoke Ulaya, Je, ni nini sababu za kuenea huku…haujakusudia bwana Rashidi kinyume cha mazoea yako?!

Rashidi: Bila shaka mimi ni mwenye kufurahi kwa ninayosikia, kwa hiyo nimechagua kunyamaza ili nizidi kusikiliza….kwa mtazamo wangu kuna sababu ndani ya Uislamu wenyewe, na kwa sababu ya jamii yenyewe ya Magharibi, na sababu zingine za mazingira: Na vipengele vingine vyenye kuchangia kusambaa kwa Uislamu…. Lakini nitaashiria kuwa hilo sio geni kwa dini kongwe, mizizi yake imesambaa na kunyooka tokea kuumbwa kwa mwanadamu, tokea Adam (‘Alayhi salaam), wala mzizi huu wa kihistoria hadi hivi sasa haujakatika.

Maiko: Hata hivyo bwana Rashidi sisi tunajua kuwa Uislamu haujadhihiri isipokuwa miaka elfu moja na mia nne tu iliyopita, na kama unavyojua kuwa kuna dini zingine za mbinguni, kama vile Ukristo na Uyahudi au utapinga hilo?!

Rashidi: Kuna ufahamu katika jambo hili unapaswa kusahihishwa, nao ni kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni moja na sio nyingi, moja kwa sababu inatoka katika chanzo kimoja, nacho ni kutoka kwa Allah (Mungu Mmoja) aliyeumba viumbe vyote, lakini kuna baadhi za hali ambazo huchungwa na dini hii moja inapelekea uwepo wa sheria mahsusi kwa hali hizi au katika umma mbali mbali, kama ambavyo inaweza kutokea upotofu wa dini hii kutokana na matokeo au umbali wa (wakati) kutoka kwenye chanzo cha ujumbe wenyewe, hivyo basi ikabidi kuhuisha dini kwa kutuma Mtume mpya ambae atathibitisha misingi ya dini hii, hili ndilo lililoashiriwa na hadithi ya Mtume wa Uislamu: “Manabii ni ndugu, dini yao ni moja, lakini mama zao ni wengi.” Yaani nyakati zao na sheria zao ni nyingi na zinatofauatiana, ama kilele chake kilikuwa wakati wa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na Ujumbe huu wa Mtume huyu ulikusanya vipengele vyenye kuhifadhi usalama wa dini hii na kuto kupotea, ambao umeihuisha na kurejesha katika usafi wake. Hivyo basi dini hii haitokatika na unyoofu huu wa kihistoria utaendelea hadi kuisha kwa wanadamu, kwa kuzingatia kuwa ni dini ya mwisho aliyoichagua Mwenyezi Mungu kwa wanadamu, hivyo katika hali ya kawaida ni yeye kuwaridhia wao yanaoafikiana na maumbile yao na kawaida kupata kuenea huku kukiachwa yatafanyika kwa njia ya kawaida.

Rajev: Huu ni mtazamo mpya na wenye kunisisimua, kama ni hivyo turejee pale ilipokuwa ututajie sababu za kuenea kwa Uislamu.

Rashidi: Ndio; ama sababu za dhati za Uislamu tutafupisha kuwa sifa zake ndizo zinaifanya kuenea; nazo ni:-

Ni dini nyepesi katika jengo lake, yenye undani katika maana yake, wazi kwa mtazamo wake, imeenea katika mfumo wake, mafundisho yake ni mepesi, haihitaji uwezo mkubwa wa kiakili, haina talasimu, wala siri, wala ugumu wowote.

Dini ya utu, huzungumza na maumbile ya mwanadamu na hutangamana nae katika mazingira yake, na kuitikia mahitajio yake, na kutibu kadhia zake, hujibu maswali yanayoelekezwa kwake na huunganisha katika jamii na kuthibitisha usawa uliotimia kati ya wanadamu kulingana na asili zao, juu ya tofauti walizonazo za rangi zao, ndimi zao, maarifa yao na viwango vyao vya kijamii.

Dini inayokwenda na mazingira, haiwi juu ya uhalisia wa mwanadamu wala haipotei, na kwa uhalisia huu ni dini inayokusanya baina ya dunia na akhera, wala haioni mgongano kati yake.

Dini inayoheshimu akili ya mwanadamu, na huithamini fikra ya mwanadamu na kuweka hoja za kiakili na njia za kimantiki juu ya kilele cha kufahamiana na kujadiliana katika mambo yanayofaa yenye faida.

Dini isiyopiga vita elimu na maendeleo, bali inaihamasisha, na hakika za kisayansi zilizothibitika walizofikia wanazuoni wa kisasa zinaafikiana na tafsiri ya mandiko ya Qur’an yaliyopokelewa katika nyanja zile kabla ya karne kumi na nne.

Dini inayokwenda pamoja na harakati za maendeleo, Uislamu umethibitishwa uwezo wake katika kuamiliana na mambo yenye kujitokeza na mabadliko ya kijamii ambayo yanajitokeza katika maisha kwa kutekeleza mabadiliko ya zama na mahala.

Dini yenye kumhakikishia mwanadamu uhuru wa kweli, ambao haufikiwi kwa ajili ya maana yake isipokuwa pindi mwanadamu anapompwekesha Mola wake kwa ibada ya kweli; kwa sababu ya hilo hawi mwanadamu ni mja kwa mwanadamu yeyote yule, au kwa kiumbe chochote, au mja wa kuyaabudu mazingira yake.

Dini iliyokuwepo na haitaacha kufunguka juu ya desturi zingine.

Maiko: Mimi nitakuambia sababu zilizojificha katika jamii ya Ki-magharibi.

Jamii zetu za Magharibi zinaishi katika janga la kifikra toka mwanzo wa karne iliyopita na kabla yake, na tatizo hili limejitokeza katika migongano mingi iliyoishi nayo jamii ya Magharibi, haswa baina ya kanisa na sayansi (elimu), kisha kati ya madhehebu mbali mbali ya kifalsafa na baina ya tabaka mbali mbali katika jamii tofauti, na hayo yameacha mpasuko mkubwa na babaiko, kukosekana kwa utambulisho.

Kisha baada ya hapo faragha ya kiroho ambayo inatoka kwa mwananchi wa Magharibi….faragha inayokaba roho ya mwanadamu na kuondoa hadhi yake na kushuka thamani ya mwanadamu…wakati ambapo vitu na maada vinakuwa juu ya hadhi ya mwanadamu na kufunika thamani zote za mwanadamu, kiasi cha kwenda kama vile mashine au sehemu ya mashine kubwa.

Kipengele kingine muhimu kina wakilishwa na shaka wanayoishi nayo Wamagharibi wengi kuhusu dini yao, na wanachokiona kuhusu kuwepo kwa migongano katika itikadi zao, pamoja na kasumba zilizo wazi kwao, achilia mbali yale yanayofanywa na Kanisa kwa kuzingatia kuwa ndio njia safi (tohara) na kusamehewa madhambi kwa njia ya utawa, wengi wetu wanaona kuwa ni kwenda kinyume na tabia na maumbile ya mwanadamu na kugongana nae katika mambo mengi ya maisha.

Hatuwezi kusahau kumomonyoka kwa maadili na kuparanganyika kwa familia na jamii ambayo imezikumba jamii nyingi za Magharibi.

Rashidi: Tukitaka kuzungumzia vipengele vya uhalisia, tunachokiona ni propaganda za kuupaka matope Uislamu, na kuwatesa wafuasi wake, hili linatupa kikwazo cha mtu kutaka kujua juu ya dini hii.

Kama ambavyo juhudi za wanaoita kwa Allah (wanaoutangaza Uislamu) na kuusambaza Uislamu, miongoni mwazo ni mijadala baina ya wanazuoni wa dini ya Kiislamu na dini zingine…hupelekea watu wa Magharibi kuujua Uislamu.

Usisahau athari za Waislamu wachache waliopo katika nchi za Magharibi, ambapo kuna fursa ile kwa Wamagharibi kujua kuwa ukaribu wa Uislamu kwa kuwaona Waislamu, jambo ambalo linatayarisha kuujua Uislamu na kuona namna wanavyoishi Waislamu wenyewe kiuhalisia.

Yote hayo yananipa hisia za hali nzuri ijayo inayothibitisha kuwa mustakbali ni wa dini hii.

  - viambatano za migadala ya saada
  - viambatano za simulia
  - viambatano za vitabu
  - viambatano za vidio